ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Tuesday, 18 April 2017

WANAFUNZI UDOM WATOA MSAADA HOSPITALI YA MKOA DODOMA

Dr. Leah (kushoto) Mshauri katika kitengo cha damu salama na mwenzake wakiwa wamebeba boksi lenye vifaa vilivyotolewa na UDOMSSO.
Wanafunzi wanaosoma kozi ya Sosholojia katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) waliadhimisha siku kuu ya Pasaka kwa kutoa msaada katika hospitali ya rufaa ya Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 15/04/2017 kupitia jumuia yao ya UDOMMSO (University of Dodoma Sociology Students' Organization).
Rais wa UDOMSSO Mr. James Simon (kulia) akikabithi moja ya boksi zenye vifaa vya matibabu vilivyotolewa na UDOMSSO.
Msaada uliotolewa na wanafunzi hao ni vifaa vya kimatibabu pamoja na uchangiaji wa damu wa hiari kwa baadhi ya wanafunzi hao.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Blood bags, Nasal Gastric Tubes na Blood giving sets ambavyo...
vitakuwa msaada kwa wagonjwa watakaokuwa na uhitaji wa vitu hivyo.

Baadhi ya wanasosholojia wakichangia damu
Akizungumza mbele ya Katibu wa hospitali hiyo Dokta Issack Mjuni, Rais wa UDOMSSO ndugu James Simon alisema, "Sisi kama jumuia ya Sosholojia ambao pia tunasoma kuhusiana na masuala ya kitabibu na kiafya (Medical sociology), tunaguswa sana na matatizo ambayo yanaikumba jamii kwa ujumla. Awali tulifikiria tu kuja kujitolea kufanya usafi wa mazingira ya hapa hospitalini na kutoa vizawadi kwa baadhi ya wagonjwa kama sabuni hasa kwa wodi ya akina mama waliojifungua.

Lakini baada ya ushauri  na maelezo kutoka kwa daktari mmoja hapa hospitalini kuwa kuna vifaa vya kimatibabu ambavyo huwa vinahitajika mara kwa mara huku kukiwa na changamoto ya vifaa hivyo kutosheleza kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa, na upungufu wa damu katika benki ya damu ya hospitali hiyo; tukaona ni vyema kutoa vifaa hivyo hata vikiwa vichache vikasaidie kuokoa maisha ya ndugu zetu wagonjwa ambao pengine wasingeweza hata kuitumia sabuni tuliyopanga kuwapatia hapo awali. 

Katibu wa Hospitali Dokta Issack (kushoto) akiongea na wanafunzi waliofika hospitalini hapo.
Sisi kama wanasosholojia tumekuwa tukijaribu kuwa karibu na jamii kwa kufanya shughuli mbalimbali kama upandaji wa miti na kuwatembelea watoto yatima na kutoa msaada kwao kwa kile kidogo tunachobahatika kuchangishana sisi kwa sisi", aliongeza.

Akiongea baada ya kupokea msaada huo, Dokta Issack aliwashukuru sana wanafunzi hao wa Sosholojia kwa kitendo hicho cha kiungwana, na upendo waliouonesha kwa wagonjwa na hata kwa serikali. "Kwa niaba ya Serikali, ninawashukuru sana kwa moyo wenu wa kujitolea na upendo mliouonesha kwa kuja kututembelea na kutoa msaada huu. Naamini utakuwa ni msaada mkubwa. Nawatakia kila la heri na mafanikio katika masomo yenu, Mungu awaepushe na "SAP" (supplementary) katika masomo yenu," alisema Dokta Issack ambaye pia ni katibu wa hospitali hiyo.

Dr. Leah (aliyesimama) akitoa mafunzo ya uchangiaji damu kwa wanafunzi waliofika hospitalini hapo.
Naye Mshauri wa Damu salama Dokta Leah, aliwashukuru wanafunzi kwa moyo wao wa kujitoa na ujasiri wa kuchangia damu. "Huwa tunapata shida sana ya damu, wagonjwa wanaohitaji damu wanakuwa wengi lakini benki ya damu wakati mwingine inakuwa haina damu. Kwa mliojitolea damu nasema asanteni sana; naamini mmeokoa maisha ya watu. Tunawaomba muendelee na moyo huo huo wa ujasiri na upendo na uzalendo. Mungu awabariki sana mfaulu vizuri katika masomo yenu.

No comments:

Post a Comment