Jumuia ya wanafunzi wanaosoma Sosholojia katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOMSSO) leo wamezindua Blog hii na kuiweka rasmi katika mfumo ambao kila mtu anaweza kusoma kilichochapishwa katika Blog hii (Public readers).
Uzinduzi huo umefanyika katika mkutano mkuu (general assembly) wa wanafunzi wote wanaosoma sosholojia katika chuo kikuu cha Dodoma katika ukumbi wa theatre one, skuli ya humanities na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa jumuia hiyo pamoja na wanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza, hadi wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia. Mkutano huo pia uliweza kuhudhuliwa na Mkuu wa Idara ya Sosholojia na Anthropolojia Dokta Nelson Ishengoma....endelea..
![]() |
| Mkuu wa Idara ya sosholojia Dr. Ishengoma akizindua rasmi Blog ya UDOMSSO na kuiweka "Public" |
Uzinduzi huo umefanyika katika mkutano mkuu (general assembly) wa wanafunzi wote wanaosoma sosholojia katika chuo kikuu cha Dodoma katika ukumbi wa theatre one, skuli ya humanities na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa jumuia hiyo pamoja na wanafunzi kuanzia mwaka wa kwanza, hadi wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia. Mkutano huo pia uliweza kuhudhuliwa na Mkuu wa Idara ya Sosholojia na Anthropolojia Dokta Nelson Ishengoma....endelea..
| Mwenyekiti wa UDOMSSO ndugu James Simon |
Aidha, Katibu mkuu wa UDOMSSO ndugu Stanley Mellack akitoa maelezo juu ya Blog alisema kuwa Blog ina faida nyingi kwa Organization, na kwa jamii pia. Miongoni mwa faida hizo Katibu mkuu ndugu Mellack amesema kuwa UDOMSSO inaweza kujipatia kipato kupitia matangazo ya kibiashara ambayo makampuni yanaweza yakavutiwa na Blog na kuamua kutangaza biashara zao kupitia Blog hii.
Faida nyingine ni kuleta mabadiliko katika jamii ambapo amesema kuwa habari inayochapishwa kwenye blog kama ilivyo
mitandao mingine ya kijamii inaweza kusaidia kuibadilisha jamii kwa nyanja
mbalimbali kama vile kutoa elimu juu ya jambo fulani, kuhamasisha maendeleo, na
kubadilisha mtazamo wa jamii kubwa ya watu watakaosoma machapisho ya blog hii.
Lakini pia akaongeza kuwa Blog ni nyenzo muhimu ya kuitangaza UDOMSSO mahali popote duniani kwakuwa blog inaweza kutazamwa na mtu yeyote duniani
kote na kusoma machapisho (posts) yaliyopo.
Aidha katibu huyo hakusita kuzitaja athari zinazoweza kuletwa na matumizi mabaya ya blog kama vile kusababisha vurugu miongoni mwa wanajamii,
uchochezi kama vile wa kisiasa na kidini,na mambo mengine yanayoweza
kusababisha kutoweka kwa amani.
![]() |
| Kuu wa Idara ya Sosholojia Dr. Nelson Ishengoma |
![]() |
| Mwenyekiti wa UDOMSSO (kulia) na Mkuu wa Idara |

No comments:
Post a Comment