ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Thursday, 13 April 2017

KISA CHA KWELI: HUYU NDO MBWA MWENYE UPENDO WA DHATI KULIKO WANYAMA NA WATU WENGI


Anaitwa HACHIKO, ndiye mbwa anayeaminiwa kuwa na upendo wa dhati na mtiifu kuliko mbwa wengine duniani. Alizaliwa Novemba 10, 1923 nchini Japan katika jiji la Tokyo. Umaarufu wake duniani ulitokana na heshima, upendo wa dhati na utii kwa Bosi wake Hidesaburo Ueno aliyekuwa Profesa katika idara ya kilimo katika chuo kikuu cha Tokyo nchini Japan.

Hachiko enzi za uhai wake

Kila mara Hachiko alikuwa akimsindikiza Bosi wake katika kituo cha treni cha Shibuya (Shibuya station) alipokuwa akipanda treni na kuelekea kazini. Mbwa huyo alihakikisha Profesa Hidesaburo amepanda treni na kuondoka ndipo na yeye anarudi nyumbani. Tofauti na wengi tusiozingatia muda; kila ilipofika jioni, Hachiko aliwahi stesheni kumpokea Bosi wake katika kituo cha Shibuya kwani alijua vyema muda wa treni kuwasili. Alifanya hivyo kila siku ambayo Bosi wake alitoka kwenda kazini na kuzidi kujizolea umaarufu. Siku moja mwezi Mei 1925 alimsindikiza Bosi wake stesheni ya Shibuya kama kawaida yake bosi alipokuwa akienda kazini. Jioni kama ilivyokuwa ada aliwahi stesheni kumpokea. Hata hivyo treni ilipowasili,.....
abiria wote waliteremka lakini Hachiko hakumuona Bosi wake akiteremka.
Picha ya mwisho ya hachiko akiwa amekufa,wa pili kutoka kuliawalio chuchumaa ni mke wa Profesa Hidesaburo na baadhi ya staff wa stesheni ya Shibuya wakiomboleza.
Alikaa hapo stesheni kwa muda na baadaye alikata tamaa na kurudi nyumbani akiwa ni mwenye huzuni.Siku hiyo Profesa Ueno akiwa kazini alipatwa na ugonjwa na muda mfupi tu alifariki akiwa hukohuko kazini. Hachiko aliendelea kufika stesheni kila jioni treni ilipowasili kuona kama atamwona Bosi wake akiteremka lakini alirejea nyumbani peke yake. Miaka na miaka ilizidi kwenda lakini Hachiko hakukata tamaa ya kwenda stesheni ya Shibuya kumsubiria Bosi wake kwani aliamini ipo siku Bosi atarejea na atarudi naye nyumbani. Machi 8, 1935 Hachiko alifariki dunia akiwa maeneo ya stesheni msubiri Bosi wake Profesa Hidesaburo Ueno ikiwa ni miaka karibia 10 tangu afariki dunia. Baadaye madaktari walitoa taarifa kuwa Hachiko alikufa kwa ugonjwa wa kansa. Hachiko alileta simanzi miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia maisha yake. Lilijengwa sanamu la Hachiko hapo stesheni ya Shibuya, pia ulijengwa mnara wa Hachiko pembezoni mwa kaburi la Profesa Ueno lililopo katika makaburi ya Aoyama.

No comments:

Post a Comment