ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Wednesday, 14 March 2018

POLISI: NONDO ALIJITEKA MWENYEWE.


TSNP: TAARIFA ZA KILICHOMSIBU NONDO ZINAKINZANA.
Kamanda Mambosasa akiwa na Nondo


Dar es salaam. Jeshi la polisi kupitia kwa kwa Kamanda Mambosasa limedai kuwa mwanafunzi wa chou kikuu cha Dar es salaa (NONDO) ambaye alidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana; hakutekwa na mtu yoyote labda alijiteka yeye mwenyewe. Taarifa za kutekwa kwa Nondo ambaye pia ni mwenyekiti wa mtandao  wa wanafunzi Tanzania zilianza kusikika hasa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 6 Machi 2018, ambapo inadaiwa Nondo mwenyewe alimtumia ujumbe wa simu (sms) Rafiki yake usiku wa manane akidai kuwa yuko kwenye hatari kubwa (I am at high risk).

Akiongea mbele ya waandishi wa habari Kamanda Mambosasa

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO, JUMATANO MARCH 14, 2018.

Click on a Newspaper to Zoom In... and Out....

Monday, 26 February 2018

HIZI NDIZO FEDHA ZENYE THAMANI NDOGO ZAIDI DUNIANI.

Ukizungumzia thamani ya pesa, watu wengi hupenda kujua na kufuatilia zaidi fedha zenye thamani kubwa zaidi. Na hapa zitatajwa fedha kama vile Paundi ya Uingereza, Euro, Dola ya Kimarekani na nyingine zenye thamani kubwa kama hizo.

Lakini Je, unazijua fedha zenye thamani ya chini kabisa ulimwenguni? Hizi hapa ni Chache kati ya hizo.

Thursday, 14 December 2017

NI KWELI WANANUNULIWA AU KUNA KITU CHADEMA?

Msikilize hapa alichokizungumza Mbunge wa Siha kupitia CHADEMA Dr. Molel mara baada ya kujiuzulu nafasi ya ubunge na kujiunga na CCM. Ikumbukwe ni siku chache tu baada ya mbunge wa Kinondoni kupitia CUF (Maulid Mtulia) kujiuzulu na kuhamia CCM. Ni katika mfululizo wa Viongozi na wakereketwa mbalimbali kutoka vyama vya upinzani kuvihama vyama vyao na kujiunga na chama tawala cha CCM.


MAGUFULI AGOMA KUZIKWA DODOMA, ARUDISHA ARDHI KWA WANANCHI.

Rais Magufuli amerudisha ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekali 100 kwa wananchi mjini Dodoma na kusema kuwa yeye atakapokufa asizikwe mjini Dodoma. Eneo hilo lilitengwa na serikali kwa ajili ya maziko ya viongozi mjini hapo lakini viongozi wengi wamekuwa wakipendelea zaidi kuzikwa kwao. Magufuli ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa nyumba za Iyumbu mkoani Dodoma."Mimi nimeshasema nikifa nazikwe kule nyumbani alikozikwa....

Saturday, 9 December 2017

BABU SEYA NA MWANAE WAPATA UHURU SIKU YA UHURU.

Babu Seya akiwa na mwanaye Papii Kocha
Shangwe na nderemo vimesikika kutokakwa Watanzania walio maeneo tofauti tofauti ya nchi ya Tanzania hususani waliokuwepo ndani ya uwanja wa Jamhuri yalipo makao makuu ya Tanzania Dodoma na wale waliokuwa majumbani wakifuatilia sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9/12/1961. Shangwe hizo kubwa zilitokana na kauli ya mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli ambaye mbali na kusamehe wafungwa 8157 leo

Friday, 8 September 2017

TUNDU LISU AHAMISHIWA NAIROBI, AFYA YAKE INATIA MOYO


Tundu Lisu

Tukio la kupigwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu (Chadema) na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake jana mchana limeendelea kulaaniwa vikali na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii na media nyinginezo.

Lissu akiwa amefika nyumbani kwake Area D, eneo la Site Three, baada ya kuahirishwa kwa kikao cha bunge, kabla hajashuka kwenye gari watu wasiojulikana wakiwa kwenye gari linalodaiwa kuwa ni aina ya Nisani ambalo namba zake hazikutambulika, walianza kumshambulia kwa risasi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto, risasi

DOGO MTEKAJI WA WATOTO AUAWA AKIJARIBU KUWATOROKA ASKALI.



Peter Samson, Mtuhumiwa wa utekaji wa watoto

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema Peter aliuawa na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka eneo la Mkonoo, Kata ya Muriet jijini Arusha.

Peter Samson mwenye umri wa miaka 18 ni dogo kiumri lakini ni mtuhumiwa wa vitendo vya utekaji wa watoto jijini Arusha. Kijana Peter ambaye imebainika alikuwa akiishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha, ameuawa wakati