ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Thursday, 18 May 2017

FUMANIZI LA WANAFUNZI LASABABISHA TAHARUKI UDOM

Wasichana wawili wanafunzi wa UDOM wamesababisha watu kuzizima kwa kelele na miruzi iliyoambatana na zomeazome baada ya kutaka kutoana ngeu kwa kile kilichotajwa kuwa ni mapenzi. Akina dada hao wakazi wa block 1 college ya Humanities wamejikuta katika kasheshe hilo baada ya kugundua kuwa wanamtumikia Bwana mmoja kinyume na mategemeo yao. Wapasha habari wa tukio hilo wanadai kuwa; Akiwa anajiamini na bila kujua, mmoja wa wanafunzi hao amefika hostel block 6 ambayo inakaliwa na wanaume kwa lengo la kumtembelea mwenzie (mpenzi wake) lakini akastaajabu kumkuta akiwa na msichana mwingine katika mazingira yaliyomtia wasiwasi na kuhisi anaibiwa. Aidha, aliyekutwa naye alijikuta akistaajabu tukio hilo kwani aliamini yuko sehemu salama na peke yake. Uzalendo ulipowashinda walianza kumiminiana maneno makali makali huku
kila mmoja akilalamika kuvamiwa kwenye miliki yake.

Tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa mbili na nusu za usiku limevuta hisia za watu waliokuwa eneo hilo na ndipo wengine wakaanza kupiga kelele za kishabiki na zomeazomea. Hali hiyo imewafanya hata wengine waliokuwa vyumbani mwao na katika hostel nyingine kuanza kupiga kelele bila hata ya kujua kinachoendelea. Ndani ya muda mchache tu block zote za 5,6,7,8 na nyingine za jirani zilitawaliwa na kelele ambazo zilisababishe wengine kuhisi kuna tatizo limetokea na hivyo kuteremka kutoka ghorofani na kuja chini kabisa huku wakiulizia tatizo lililopo. Wengi wakiwa wametoa vichwa madirishani kuangalia nini kilikuwa kikiendelea nje, wengine walianza kuokota mawe na kukimbilia ulipokuwa umati wa watu waliokuwa wakiendelea kuwazonga akina dada hao.

 Fujo zilipozidi ndipo akina dada hao walipoamua kuondoka na kurejea hostel kwao block 1 huku umati mkubwa ukiwafuata, kuwazongazonga, kuwazomea na kuendelea kupiga kelele kitu kilichosababisha hata wakazi wa block zilizo mbali kukimbilia kule walikoona watu wakipakimbilia ili kujua ni nini kilikuwa kikisababisha kelele hizo na wengine wakiwa na silaha za mawe wakiamini ni mwizi amekamatwa. Jitihada za walinzi kuwasaidia akina dada hao zilishindikana kwani umati wa watu ulikuwa mkubwa hadi pale baadhi ya viongozi wa wanafunzi kwa kushirikiana na wanafunzi wengine walipowapeleka akina dada hao hostelini kwao na kuzuia mlango wa kuingilia watu watu wasiwafuate. 

Wanafunzi wengine wakasikika wakilaumu kwa kuficha mwizi huku wakitaka atolewe nje ili wamuadhibu ndipo viongozi hao wakawaambia kuwa siyo wezi bali wamefumaniana kwa mwanaume mmoja ambaye kila mmoja aliamini ni wa kwake. Baada ya kupewa taaraifa hiyo wengine waliondoka huku wanasononeka kupoteza muda wao kwa mambo ya kijinga na wengine wakitukana. Aidha wengine walibaki wakicheka na wengine wakiwa wanadai watolewe hivyo hivyo wazione sura zao ambapo hata hivyo viongozi hao waligoma kufuata matakwa ya umati huo uliofulika katika ukumbi wa block 1.

No comments:

Post a Comment