ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Sunday, 25 June 2017

UDOMSSO YAPATA VIONGOZI WAPYA

Ndugu Gerald Bundala, Rais mteule wa UDOMSSO
Jumuia ya wanafunzi wanaosoma sociology katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOMSSO) imepata viongozi wapya wa kuiongoza jumuia hiyo kubwa ya wanafunzi chuoni hapo. Mchakato wa kupata viongozi wapya ulianza wiki mbili kabla ya tarehe ya uchaguzi ambapo wagombea walijitokeza kuchukua form za kugombea katika nafasi tofauti tofauti.


Katika uchaguzi huo uliofanyika tarehe 10/6/2017, viongozi kadhaa waliweza kutangazwa kuwa washindi wa nafasi walizokuwa wakiwania katika kuiongoza jumuiya hii. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi hiyo Bwana Edward Mdaki kwa kushirikiana na wanatume wengine Luciana Daudi, Msafiri Ponera na Ally Hafidh katika kusimamia uchaguzi huo; alimtangaza Bwana Gerald Bundala aliyekuwa Katibu Msaidizi wa jumuiya hiyo katika awamu iliyopita kuwa Rais mpya wa UDOMSSO. Aidha nafasi ya Rais msaidizi alichaguliwa
ndugu John Umbege.

Ndugu John Umbege, Makamu wa Rais mteule
Nafasi ya Katibu mkuu ilitangazwa kushikwa na aliyekuwa Afisa habari wa Jumuiya hiyo katika uongozi uliomaliza muda wake mwanadada Aginatha  Matungwa atakayesaidiwa na (katibu msaidizi) ndugu Peter Kibwana.

Aginatha Matungwa, Katibu mkuu mteule
Katika nafasi ya Uhasibu, Tume ilimtangaza Bwana Isihaka Mgalawe kama mhasibu mkuu wa jumuiya na atasaidiwa na mwanadada Eva Ringo (mhasibu msaidizi) wa jumuiya. Kwa mujibu wa katiba ya UDOMSSO, Rais wa Jumuiya anayo mamlaka ya kuteua viongozi wengine wa jumuiya watakaokuwa katika kamati mbambali za Jumuiya kama vile, kamati ya habari (afisa habari), kamati ya taaluma, nidhamu nk. ambao majina yao yako kwenye orodha ya viongozi.

Mwenyekiti wa Tume ndugu Edward Mdaki alitoa rai kwa wanasosholojia wote kushirikiana na viongozi wote wapya waliochaguliwa bila kujali ulimpigia kura ama la. Kwakuwa wao ndo washindi basi watakuwa ni viongozi wa wanafunzi wote na si wa waliowapigia kula pekee.

Ndugu Isihaka Mgalawe, Mhasibu Mkuu mteule
Aidha Rais aliyemaliza muda wake ndugu James Simon na aliyekuwa Makamu wa Rais wa jumuiya hiyo kabla ya uongozi uliomaliza muda wake ndugu Rashid Mirambo, waliwataka wanasosholojia wote kuwa kitu kimoja na kupendana wao kwa wao na kuwapenda viongozi wao huku wakiwapa ushirikiano wa kutosha katika masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo. "Uongozi ni mgumu, mnapaswa kushirikiana vizuri katika mazingira yote ya shida na raha na muwe na kuvumiliana kwa mapungufu mbalimbali yanayojitokeza", aliwahusia ndugu Rashid Mirambo aliyewahi kuwa Makamu wa Rais.
 Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Bwana Edward Mdaki, na wanatume wengine Msafiri Ponera (katikati) na Ally Hafidh kulia
Kwa upande wa Rais aliyemaliza muda wake ndugu James Simon aliwakumbusha wanasosholojia kuwa wao ni kitu kimoja, lengo lao ni moja, nalo ni kuijenga UDOMSSO moja na kusaidiana katika masomo na kuisaidia jamii kwa namna tofauti tofauti.

Naye Rais mteule wa Jumuiya ndugu Gerald Bundala aliwaomba wanafunzi wote wa sociology kushirikiana na viongozi wapya na kuahidi kuwatumikia wanajumuiya kwa namna mbalimbali na kuwaleta wote pamoja na kuwa kitu kimoja bila kujali kuwa huyu yuko mwaka wa kwanza, wa pili au wa tatu.

No comments:

Post a Comment