ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Friday, 8 September 2017

NI MADINI TENA! HAYAJAMWACHA MTU SALAMA!


Waziri Simbachawene
Madini ya Tanzanite

Ripoti za kamati za uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi zilizoundwa na spika wa Bunge Job Ndugai ziliwasilishwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ndugu Kassim Majariwa mikononi mwa rais Magufuli jana Ikulu jijini Dar es salaam. Ripoti hizo zimewataja baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, James Mdoe; Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi, Mawasiliano Edwin Ngonyani na wengine.

Baada ya kupokea ripoti hiyo,
Rais Magufuli amewataka wateule wake wote waliotajwa katika ripoti za kamati zilizotathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya tanzanite na almasi kukaa pembeni kupisha vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi zake.

Katika kutii agizo la Rais Magufuli;Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo baada ya kutajwa katika ripoti za uchunguzi wa biashara ya madini ya Tanzanite na Almasi iliyoonyesha namna serikali lilivyopoteza matrilioni ya fedha kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha, Simbachawene amedai kuwa ametajwa kuhusika kwakuwa alikuwa ni mmoja wa watendaji na hivyo ni kama ajari tu lakini hakuwa na lengo la kuihujumu nchi wala kuiletea nchi hasara iliyotajwa katika ripoti hiyo. Magufuli ameagiza kukamatwa kwa watakaobainika na kulitia ama kulisababishia taifa  na wachukuliwa hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment