ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Friday, 8 September 2017

DOGO MTEKAJI WA WATOTO AUAWA AKIJARIBU KUWATOROKA ASKALI.



Peter Samson, Mtuhumiwa wa utekaji wa watoto

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema Peter aliuawa na askari polisi wakati akijaribu kuwatoroka eneo la Mkonoo, Kata ya Muriet jijini Arusha.

Peter Samson mwenye umri wa miaka 18 ni dogo kiumri lakini ni mtuhumiwa wa vitendo vya utekaji wa watoto jijini Arusha. Kijana Peter ambaye imebainika alikuwa akiishi na kaka yake ambaye ni askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha, ameuawa wakati
alipojaribu kuwatoroka polisi eneo la Mkonoo jijini Arusha.

Aliuawa na Jeshi la Polisi jana, akiwa chini ya ulinzi wakati alipokwenda kuwaonesha askari alipo mtuhumiwa mwingine waliyeshirikiana kuteka watoto kadhaa na wengine wawili kufa kwa kuwatumbukiza ndani ya shimo la maji taka.
“Samson alijaribu kutoroka kabla ya kuonesha mtuhumiwa mwenziwe, lakini polisi wetu walikuwa imara walimpiga risasi miguu yote miwili na kufariki".

Kamanda Mkumbo alisema Peter alitoa ushirikiano kwa Polisi na kuamua kwenda kuwaonesha mshirika mwenzake lakini kabla hawajafika eneo husika na kuonesha mshirika mwenzake ghafla alitaka kuwatoroka polisi hao na ndipo walipoamua kumpiga risasi miguu yote miwili na kumkamata kisha kumkimbiza hospitali ya Mount Meru ambapo uamauti ullimkuta.

No comments:

Post a Comment