ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Saturday, 9 December 2017

BABU SEYA NA MWANAE WAPATA UHURU SIKU YA UHURU.

Babu Seya akiwa na mwanaye Papii Kocha
Shangwe na nderemo vimesikika kutokakwa Watanzania walio maeneo tofauti tofauti ya nchi ya Tanzania hususani waliokuwepo ndani ya uwanja wa Jamhuri yalipo makao makuu ya Tanzania Dodoma na wale waliokuwa majumbani wakifuatilia sherehe za kuadhimisha miaka 56 ya kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika uliopatikana tarehe 9/12/1961. Shangwe hizo kubwa zilitokana na kauli ya mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli ambaye mbali na kusamehe wafungwa 8157 leo
katika sherehe hizo, Jina la Babu Seya limeibua shangwe za aina yake. 

Rais Magufuli amemsamehe Babu Seya ambaye jina lake halisi ni Viking Nguza na Mtoto wake aitwaye Jonhson Nguza maarufu ka Papii Kocha ambao wote ni wasanii waliokuwa wamefungwa gerezani kwa miaka kadhaa kwa kosa la jinai. Mbali na kukata rufaa mara nyingi lakini Babu Seya na mwanae Papii Kocha hawakuweza kushinda kesi yao iliyokuwa ikiwakabili. 

Rais Magufuli ametaja idadi ya wafungwa waliopo Tanzania hadi kufikia jana kuwa ni 39,000 ambapo kati ya hao wanaume ni 37,000 na wanawake ni 2000 pekee. Kati ya wafungwa wote hao, wafungwa waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa ni 522 ambapo wanaume ni 503 wakati wanawake ni 22 tu. Aidha wafungwa 666 walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha ambapo kati ya hao wanaume ni 655 na wanawake ni 11.

Msamaha uliotolewa na Rais Magufuli ni kwa wafungwa 8157 pekee na kati ya hao wafungwa 1828 wanapaswa watolewe leo huku wengine waliobaki wakipunguziwa adhabu ama wakisubiri taratibu za wao kutoka. Rais Magufuli pia amewasamehe wafungwa 61 kati ya wale waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa.

No comments:

Post a Comment