Rais Magufuli amerudisha ardhi yenye ukubwa wa zaidi ya ekali 100 kwa wananchi mjini Dodoma na kusema kuwa yeye atakapokufa asizikwe mjini Dodoma. Eneo hilo lilitengwa na serikali kwa ajili ya maziko ya viongozi mjini hapo lakini viongozi wengi wamekuwa wakipendelea zaidi kuzikwa kwao. Magufuli ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa nyumba za Iyumbu mkoani Dodoma."Mimi nimeshasema nikifa nazikwe kule nyumbani alikozikwa....
baba "chato", yaani nizikwe hapa kwa wagogo halafu waanze kuchezea hapo na fisi zao? alisema Rais Magufuli. Aidha Magufuli amesema kuwa amejaribu na kuuliza baadhi ya viongozi wastaafu iwapo kama wanataka kuzikwa Dodoma watakapo fariki lakini kila mmoja akataka azikwe kwao.
"Nilishatoa maagizo hiyo sheria tuibadilishe. Wakati tukisubiri hiyo sheria tuibadilishe natamka hapa, hii ardhi tunawarudishia wananchi wenyewe, "alisema Rais Magufuli". Magufuli amewaagiza wakazi wa Iyumbu kuanza kuilima na kujenga katika ardhi hiyo na watakaokuja kuitaka hiyo ardhi watalipa fidia kwa mujibu wa sheria namba 3(g).

No comments:
Post a Comment