![]() |
| Kamanda Mambosasa akiwa na Nondo |
Dar es salaam. Jeshi la polisi kupitia kwa kwa Kamanda
Mambosasa limedai kuwa mwanafunzi wa chou kikuu cha Dar es salaa (NONDO) ambaye
alidaiwa kutekwa na watu wasiojulikana; hakutekwa na mtu yoyote labda alijiteka
yeye mwenyewe. Taarifa za kutekwa kwa Nondo ambaye pia ni mwenyekiti wa
mtandao wa wanafunzi Tanzania zilianza
kusikika hasa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 6 Machi 2018, ambapo inadaiwa
Nondo mwenyewe alimtumia ujumbe wa simu (sms) Rafiki yake usiku wa manane
akidai kuwa yuko kwenye hatari kubwa (I am at high risk).
Akiongea mbele ya waandishi wa habari Kamanda Mambosasa
jana alisema kuwa uchunguzi wao (polisi) umebaini kuwa Nondo alikuwa anatafuta kiki tu kwa maslahi yake mwenyewe anayoyajua. Aidha Mambosasa alitanabaisha mbele ya waandishi wa habari kuwa, uchunguzi unaonesha kwamba kiongozi huyo wa mtandao wa wanafunzi Tanzania alienda Iringa kwa mpenzi wake. Kupitia mawasiliano ya simu ya mkononi ya Nondo, polisi iliweza kugundua kuwa baada ya kutuma ujumbe kwa Rafiki yake kuwa yuko katika hatari kubwa, Nondo aliendelea kuwasiliana na mpenzi wake huyo kitu kinachoashiria kuwa huru.

Nondo alionekana mjini Iringa akiwa hana tatizo lolote
linaloonesha kupigwa au kuumizwa Kimwili na wala Nondo mwenyewe hakuripoti
tukio hilo popote; si polisi wa kwa mjumbe baada ya kuachiwa huru na watekaji
bali alikuwa akiendelea na shughuli zake tu mkoani hapo. Mara baada ya
uchunguzi kukamilika Mambosasa alisema kuwa Nondo atapelekwa mahakamani
kutokana na taarifa hizo za uongo zilizoleta taharuki mitaani.
Kwa upande mwingine mtandao wa wanafunzi nchini Tanzania
umesema kuwa taarifa za nini hasa kilichomsibu Nondo zinakinzana. “Sisi bado hatuamini
uchunguzi uliofanywa na polisi kwakuwa hatujamsikia Nondo akiongea; na kile
kilichoelezwa na polisi mkoani Iringa na hiki tulichokisikia leo kwa polisi Dar
es salaam haviendani”, alisema msemaji wa TSNP Hellen Sisya akiiambia BBC.

No comments:
Post a Comment