ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Tuesday, 9 May 2017

TEMBO WAVAMIA UDOM

Katika hali ya kukashangaza alfajiri ya leo Tembo wamevamia katika maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) na kuzua wasiwasi miongoni mwa wanafunzi na jamii zinazokizunguka chuo hicho. Wakati wakijiandaa kwenda madarasani, baadhi ya wanafunzi walishangaa kuona kundi la tembo wanne wakiwa wanazunguka zunguka katika vichaka vilivyopo maeneo ya UDOM jirani kabisa na hostel za wanafunzi na kutoa taarifa kwa wanafunzi wengine na hivyo kutokea kundi kubwa la wanafunzi waliokuwa wakiwatazama kwa mbali huku wengine wakihofia kuwa tembo hao wanaweza wakazivamia hostel na kuwadhuru wanafunzi au
wananchiwanaokizunguka chuo.

Taarifa za uwepo wa tembo hao zilisambaa kwa kasi sana ikisaidiwa na uwepo wa mitandao ya kijamii ambapo hata wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Dodoma walifika maeneo ya UDOM ili kuwashuhudia tembo hao. Hata hivyo askari wa wanyama pori nao waliwahi kuzipata taarifa hizo na kufika eneo la tukio ambapo waliwazuia wanafunzi na wananchi kusogea zaidi walipo tembo hao.
Kwa upande wake Meneja wa mawasiliano wa shirika la hifadhi TANAPA Paschal Shelutete akiwa UDOM amesema kuwa tafiti zimeshathibitisha kuwa tembo ni mnyama anayeweza kutunza kumbukumbu kwa kipindi kirefu, na Dodoma ipo katikati ya hifadhi za Ruaha, Mikumi na pori la akiba la Swagaswaga; kwahiyo ni mapito ya wanyamapori. "Njia aliyopita tembo leo, miaka hamsini ijayo bado ataweza kukumbuka kwamba aliweza kupita njia hii, alifika kituo flani akapumzika na atafanya hivyo hivyo baada ya miaka 30, 40 au 50 ijayo.

Hivyo kwa tukio hili la leo inaaminika kuwa miaka kadhaa kama 30,40,50 iliyopita haya yalikuwa mapito ya wanyamapori wakiwemo tembo", alisema Bwana Paschal Shelutete na kuongeza kuwa zitafanyika taratibu ili kuona ni namna gani watawaondoa tembo hao katikati ya makazi ya watu bila kuleta madhara.

No comments:

Post a Comment