![]() |
| Flora akifunga ndoa na mumewe mpya Daudi Kusweka |
Emmanuel
Mbasha kwa wakati wake alikaririwa na watu akimtuhumu mkewe Flora kwa kumsaliti
kwa Gwajima huku Flora akikaririwa pia kumtuhumu
mmewe kwa kumsaliti kwa mdogo
wake Frola (shemeji wa Mbasha).
![]() |
| Flora na mume wake mpya wakiingia ukumbini |
Sintofahamu
hiyo ilifanya wanandoa hao wa kipindi hicho kujikuta katika magazeti na habari
zao kuzungumzwa zaidi katika mitandao ya kijamii kila kunapokucha. Watu wengi
walitafakari na kujiuliza maswali juu ya uhalali wa ndoa hiyo kuvunjika hasa
ukizingatia wote ni watumishi wa Mungu waliotuhubiria upendo kupitia nyimbo.
Moja ya nyimbo hizo ni "Maisha ya ndoa" ambapo ndani ya wimbo huo
Flora anakubali kwa kusema "maisha ya ndoa hufananishwa na safari ambayo
njiani kuna mambo mengi". Pamoja na hayo yote Flora anaapa kumpenda mpenzi
wake kwakuwa amemchagua kuwa wake na kwamba hataacha kumpenda maishani
mwake mwote.
Akiwa
bado hajatoka vinywani na katika bongo za walio wengi na hata katika magazeti
na mitandao ya kijamii kwa suala la talaka; Flora Mbasha amekuwa tena lulu
katika maeneo yote hayo baada ya kufunga ndoa ya pili jijini Mwanza tarehe
30/05/ 2017 na aliyekuwa mchumba wake Daudi Kusweka baada ya kuachana na
Mbasha.
Tukio
hilo limekuwa ni lulu mitaani kote huku likiigawa jamii katika pande mbili.
Wapo wanaosema kuwa ni ndoa haramu na wengine wakidai kuwa ni halali hivyo
kuzua ubishani mkubwa kati ya pande hizo mbili na wote wakitumia maandiko
matakatifu kutoka katika kitabu cha Biblia.
BIBLIA
INASEMAJE KUHUSU TALAKA NA NDOA YA MARA YA PILI?
Wengi wanaosema ni halali wamenukuu
maneno kutoka katika kitabu cha Torati sura ya 24 na msitari wa kwanza na wa
pili (Kumbukumbu yaTorati 24:1-2) 1."mtu akiisha kutwaa mke wa kumuoa,
asipopata kibali machoni mwake, kwakuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie
hati ya kumuacha, akamtilie mikononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake. 2.
Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu
mwingine".
Mathayo
5:31 pia inasema, "imenenwa pia, mtu akimwacha mkewe na ampe hati ya
talaka". Maneno haya na mengine kama haya katika Biblia huwapa nguvu
wanao kubaliana na swala la talaka na kuoa tena.
Kwa upande wa wanaopinga talaka na ndoa ya mara ya pili hutumia pia vifungu mbalimbali kutetea hoja kama vile (Marko 10:11 na12) 1."akawaambia, kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake. 2.na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine,azini". Wakorinto wa kwanza 7:10-11 inasema, 1."lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; 2. lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe".
(Marko
10:2-9) inasema "2.basi mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! ni
halali mtu kumwacha mkewe? huku wakimjaribu. 3. naye akawaambia, Musa aliwaamuru
nini? 4.wakasema Musa alitoa ruhusa ya kuandika hati ya talaka na kumuacha.
5.Yesu akawaambia, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
6.lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mke na mume. 7.kwa
sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, 8.na hao
wawili watakua mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
9.basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe"
| Flora akiwa na Mumewe wa zanani Emmanuel mbasha na Mtoto wao enzi za furaha ya pamoja |
Ni
nani aliyewatenganisha Flora na Mbasha? Mchungaji aliyefungisha ndoa ya pili ya
Flora analijua andiko hili? yeye katumia andiko gani?
Lakini
pia watu wanaokubaliana na talaka na kuolewa tena kwa Flora hulifananisha suala
hilo na maneno ya kwenye Mathayo19:9 "nami nawaambia ninyi, kila mtu
atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini;
naye amwoaye yule aliyeachwa azini". Hivyo wanadai kuwa Flora na
Mbasha wameachana kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa, hivyo kuna
uasherati hapo ambao imeandikwa kwa sababu hiyo unaweza kuoa mwingine, na kama
si sababu ya uasherati ukiachana na mwenzi wako utakuwa umezini. Lakini je,
kuna tofauti gani kati ya uasherati na uzinzi? Kati ya anayefanya tendo la ndoa
nje ya ndoa yake na yule anayetenda tendo hilo akiwa bado hajaoa, ni yupi
mwasherati?
Lengo
siyo kuchambua maandiko ya kitabu hiki Kitakatifu wakiaminicho zaidi Wakristo
wala kumtuhumu Mbasha wala Flora na mumewe mpya. Lakini kama mwanajamii unaweza
kujiuliza mkaanganyiko huu unaletwa na nini?. Nani yuko sahihi na nani
anakosea? Ya Ngoswe mwachie Ngoswe, acha wenye dini yao na wenye ufahamu mzuri
wa jambo hili walieleze. Kama jamii tunapaswa kusikiliza na kufuata miongozo
inayotolewa na viongozi wenye dhamana hiyo. Lakini miongozo hiyo isipotafsiriwa
vizuri itaitumbukiza jamii katika matatizo. Wakati Mahakama inatengua ndoa ya
Flora na Mbasha, huku mchungaji mwingine akifungisha ndoa ya pili, Mbasha yeye
alikuwa bado akidai kumpenda mkewe Flora.


Ukiwa umefanya kazi maisha yako yote kujenga familia na urithi, huwezi kuruhusu kivuli cha mtu wa tatu kiiharibu katika miezi michache tu. Niligundua kuwa mabadiliko ya ghafla ya tabia ya mume wangu yalikuwa kuingiliwa kiroho, si tu mgogoro wa katikati ya maisha.
ReplyDeleteNiliwasiliana na Mystic Kakaa kwa ajili ya uingiliaji kati wa kibinafsi. Kazi yake ilikuwa ya upasuaji. Alitambua kivuli na kukiondoa kabisa bila drama yoyote ya umma. Ndani ya siku 5, umakini wa mume wangu ulirudi nyumbani kwetu na katika mustakabali wetu. Ikiwa unalinda maisha yenye thamani kubwa na unahitaji bwana anayeelewa busara, wasiliana naye kwa: dawnacuna314@gmail.com
WhatsApp: +2349046229159
Yeye ndiye kiwango cha dhahabu.
Kwa uchawi wa upatanisho wa uhusiano/ndoa.
Uchawi wa kumfanya mpenzi wako wa zamani/mwenzi wako aombe msamaha.
Uchawi wa kumrudisha mpenzi wako/kumvutia mpenzi mpya.
Uchawi wa kurejesha mali/pesa zilizoibiwa.
Mabadiliko ya umbo/Uchawi wa kutoweka.
Uchawi wa kushinda bahati nasibu/kesi ya mahakama. Na zaidi
I want to give a testimony on how I got cured from Herpes Virus. Few months back I was having some symptoms. I went to see a doctor and many blood tests were done on me, later on I was told I had Herpes. My doctor told me that there’s no cure for Herpes. I felt bad, I went online searching for a possible cure for Herpes Virus, I saw a post of Dr. Dawn, a herbal doctor that’s helping people get cured from Herpes.Cancer.HIV and more I contacted him and told him how I’m feeling. He said his herbal medicine can cure me. He sent me the medicine via UPS delivery service and I received the medicine 6 days after he sent it, i took the medicine as prescribed by him. Before I completed the medication the symptoms stopped. I went to the doctor and carried out another blood test, surprisingly I was Negative. I haven’t had any symptoms anymore. Dr. Dawn is great and you can
ReplyDeletecontact on WhatsApp: +2349046229159
Gmail ( dawnacuna314@gmail.com )
If you need herbal medicine to cure any chronic or sexual transmitted disease's like.
HERPES.
CANCER.
HIV/AID'S and more