Hatimaye miili ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent waliopoteza maisha kufuatia ajari mbaya sana ya gari iliyokuwa imewabeba wamezikwa. Wanafunzi hao 32, waalimu wawili na dereva wa gari hiyo wameagwa kwa pamoja katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha tukio lililohudhuliwa na idadi kubwa ya waombolezaji.
 |
| Miili ya wanafunzi 32, Walimu 2 na dereva 1 ikiwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa ajili ya kuombewa na kuagwa |
endelea......
Simanzi na vilio kutoka kwa wazazi, ndugu, jamaa, marafiki na watu wengine waliofika katika tukio hilo vilitawala huku wengine wakipoteza fahamu katika viwanja hivyo.
 |
| Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent wakiwa katika majonzi mazito kwa kuwapoteza wanafunzi wenzao |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mh. Samia Hassan Suluhu aliongoza tukio hilo lililohudhuliwa pia na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa na taasisi mbalimbali.
 |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mh. Samia Hassan Suluhu akitoa heshima zake za mwisho kwa miili ya wanafunzi hao |
 |
| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Mh. Samia Hassan Suluhu akiwapa pole wazazi na ndugu wengine waliofiwa. |
 |
| Umati wa waombolezaji waliofika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
kuaga miili ya wanafunzi, walimu na Dereva waliopoteza maisha katika
ajari hiyo. |
 |
| Umati wa waombolezaji waliofika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuaga miili ya wanafunzi, walimu na Dereva waliopoteza maisha katika ajari hiyo. |
Tunawaombea Marehemu wote wapumzike kwa amani, Mungu azilaze Roho zao mahala pema peponi. Mungu awape Faraja wafiwa wote, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu.
No comments:
Post a Comment