ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Tuesday, 2 May 2017

KUFUATIA KUFUNGA NDOA MARA YA PILI; FLORA MBASHA ANAZINI? HUU HAPA WAWEZA KUWA UKWELI.

Pamoja na kwamba kwa sasa hapendi kuitwa jina la Flora Mbasha na kupendelea aitwe Madam Flora, ni ukweli usiopingika kwamba wengi watashindwa kuelewa unamzungumzia nani ukitaja Madam Flora bila kumalizia Mbasha na pengine wapo watakaofikiri kwamba unamzungumzia mtu mwingine maarufu kama yule wa kipindi cha Flora show kenye luninga.
Flora akifunga ndoa na mumewe mpya Daudi Kusweka
Mfuatano wa majina hayo mawili unajenga picha halisi ya mwanadada huyo maarufu Tanzania na nje ya Tanzania kwa nyimbo za injiri zinazowagusa wengi kama vile Jipe Moyo, Maisha ya ndoa, Alionewa Yesu, Unifiche, Fanya njia, Tanzania nakupenda, na nyingine nyingi. Licha ya umaarufu wake katika nyimbo za injiri, Flora Mbasha ametikisa vichwa vya watu na ku-make headlines za kutosha katika magazeti mbalimbali Tanzania na mitandao ya kijamii kutokana na mtikisiko ulioikumba ndoa yake na mumewe wa awali Emmanuel Mbasha. Mtikisiko huo haukuiacha ndoa hiyo salama kwani uliweza kusababisha ndoa hiyo kuvunjika mahakamani na kila mmoja kushika hamsini zake kama wasemavyo vijana mtaani. Pamoja na mengine yanayoweza kuwa sababu ya ndoa hiyo kuvunjika lakini neno usaliti kwa maana ya uzinzi umezungumzwa sana kwenye magazeti na mitandao ya kijamii kuwa chanzo kikubwa cha ndoa hiyo kuvunjika wakihusishwa watu tofauti tofauti huku Askofu Josephat Gwajima akiangaziwa zaidi na watu mbalimbali.
Emmanuel Mbasha kwa wakati wake alikaririwa na watu akimtuhumu mkewe Flora kwa kumsaliti kwa Gwajima huku Flora akikaririwa pia kumtuhumu
mmewe kwa kumsaliti kwa mdogo wake Frola (shemeji wa Mbasha).

Flora na mume wake mpya  wakiingia ukumbini
Sintofahamu hiyo ilifanya wanandoa hao wa kipindi hicho kujikuta katika magazeti na habari zao kuzungumzwa zaidi katika mitandao ya kijamii kila kunapokucha. Watu wengi walitafakari na kujiuliza maswali juu ya uhalali wa ndoa hiyo kuvunjika hasa ukizingatia wote ni watumishi wa Mungu waliotuhubiria upendo kupitia nyimbo. Moja ya nyimbo hizo ni "Maisha ya ndoa" ambapo ndani ya wimbo huo Flora anakubali kwa kusema "maisha ya ndoa hufananishwa na safari ambayo njiani kuna mambo mengi". Pamoja na hayo yote Flora anaapa kumpenda mpenzi wake kwakuwa amemchagua kuwa wake na kwamba  hataacha kumpenda maishani mwake mwote.
Akiwa bado hajatoka vinywani na katika bongo za walio wengi na hata katika magazeti na mitandao ya kijamii kwa suala la talaka; Flora Mbasha amekuwa tena lulu katika maeneo yote hayo baada ya kufunga ndoa ya pili jijini Mwanza tarehe 30/05/ 2017 na aliyekuwa mchumba wake Daudi Kusweka baada ya kuachana na Mbasha.
Tukio hilo limekuwa ni lulu mitaani kote huku likiigawa jamii katika pande mbili. Wapo wanaosema kuwa ni ndoa haramu na wengine wakidai kuwa ni halali hivyo kuzua ubishani mkubwa kati ya pande hizo mbili na wote wakitumia maandiko matakatifu kutoka katika kitabu cha Biblia.

BIBLIA INASEMAJE KUHUSU TALAKA NA NDOA YA MARA YA PILI?
Wengi wanaosema ni halali wamenukuu maneno kutoka katika kitabu cha Torati sura ya 24 na msitari wa kwanza na wa pili (Kumbukumbu yaTorati 24:1-2) 1."mtu akiisha kutwaa mke wa kumuoa, asipopata kibali machoni mwake, kwakuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumuacha, akamtilie mikononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake. 2. Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine".
 Mathayo 5:31 pia inasema, "imenenwa pia, mtu akimwacha mkewe na ampe hati ya talaka". Maneno haya na mengine kama haya katika Biblia huwapa nguvu wanao kubaliana na swala la talaka na kuoa tena.

Kwa upande wa wanaopinga talaka na ndoa ya mara ya pili hutumia pia vifungu mbalimbali kutetea hoja kama vile (Marko 10:11 na12) 1."akawaambia, kila mtu atakayemwacha mkewe na kuoa mwingine azini juu yake. 2.na mke akimwacha mumewe na kuolewa na mtu mwingine,azini". Wakorinto wa kwanza 7:10-11 inasema, 1."lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; 2. lakini ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe". 
(Marko 10:2-9) inasema "2.basi mafarisayo wakamwendea, wakamwuliza, Je! ni halali mtu kumwacha mkewe? huku wakimjaribu. 3. naye akawaambia, Musa aliwaamuru nini? 4.wakasema Musa alitoa ruhusa ya kuandika hati ya talaka na kumuacha. 5.Yesu akawaambia, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii. 6.lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mke na mume. 7.kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe, 8.na hao wawili watakua mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9.basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe"
Flora akiwa na Mumewe wa zanani Emmanuel mbasha na  Mtoto wao enzi za furaha ya pamoja
Ni nani aliyewatenganisha Flora na Mbasha? Mchungaji aliyefungisha ndoa ya pili ya Flora analijua andiko hili? yeye katumia andiko gani?
Lakini pia watu wanaokubaliana na talaka na kuolewa tena kwa Flora hulifananisha suala hilo na maneno ya kwenye Mathayo19:9 "nami nawaambia ninyi, kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini". Hivyo wanadai kuwa Flora na Mbasha wameachana kwa sababu ya kujihusisha na mapenzi nje ya ndoa, hivyo kuna uasherati hapo ambao imeandikwa kwa sababu hiyo unaweza kuoa mwingine, na kama si sababu ya uasherati ukiachana na mwenzi wako utakuwa umezini. Lakini je, kuna tofauti gani kati ya uasherati na uzinzi? Kati ya anayefanya tendo la ndoa nje ya ndoa yake na yule anayetenda tendo hilo akiwa bado hajaoa, ni yupi mwasherati?
Lengo siyo kuchambua maandiko ya kitabu hiki Kitakatifu wakiaminicho zaidi Wakristo wala kumtuhumu Mbasha wala Flora na mumewe mpya. Lakini kama mwanajamii unaweza kujiuliza mkaanganyiko huu unaletwa na nini?. Nani yuko sahihi na nani anakosea? Ya Ngoswe mwachie Ngoswe, acha wenye dini yao na wenye ufahamu mzuri wa jambo hili walieleze. Kama jamii tunapaswa kusikiliza na kufuata miongozo inayotolewa na viongozi wenye dhamana hiyo. Lakini miongozo hiyo isipotafsiriwa vizuri itaitumbukiza jamii katika matatizo. Wakati Mahakama inatengua ndoa ya Flora na Mbasha, huku mchungaji mwingine akifungisha ndoa ya pili, Mbasha yeye alikuwa bado akidai kumpenda mkewe Flora.

2 comments:

  1. Ukiwa umefanya kazi maisha yako yote kujenga familia na urithi, huwezi kuruhusu kivuli cha mtu wa tatu kiiharibu katika miezi michache tu. Niligundua kuwa mabadiliko ya ghafla ya tabia ya mume wangu yalikuwa kuingiliwa kiroho, si tu mgogoro wa katikati ya maisha.

    Niliwasiliana na Mystic Kakaa kwa ajili ya uingiliaji kati wa kibinafsi. Kazi yake ilikuwa ya upasuaji. Alitambua kivuli na kukiondoa kabisa bila drama yoyote ya umma. Ndani ya siku 5, umakini wa mume wangu ulirudi nyumbani kwetu na katika mustakabali wetu. Ikiwa unalinda maisha yenye thamani kubwa na unahitaji bwana anayeelewa busara, wasiliana naye kwa: dawnacuna314@gmail.com

    WhatsApp: +2349046229159

    Yeye ndiye kiwango cha dhahabu.
    Kwa uchawi wa upatanisho wa uhusiano/ndoa.

    Uchawi wa kumfanya mpenzi wako wa zamani/mwenzi wako aombe msamaha.

    Uchawi wa kumrudisha mpenzi wako/kumvutia mpenzi mpya.

    Uchawi wa kurejesha mali/pesa zilizoibiwa.

    Mabadiliko ya umbo/Uchawi wa kutoweka.

    Uchawi wa kushinda bahati nasibu/kesi ya mahakama. Na zaidi

    ReplyDelete
  2. I want to give a testimony on how I got cured from Herpes Virus. Few months back I was having some symptoms. I went to see a doctor and many blood tests were done on me, later on I was told I had Herpes. My doctor told me that there’s no cure for Herpes. I felt bad, I went online searching for a possible cure for Herpes Virus, I saw a post of Dr. Dawn, a herbal doctor that’s helping people get cured from Herpes.Cancer.HIV and more I contacted him and told him how I’m feeling. He said his herbal medicine can cure me. He sent me the medicine via UPS delivery service and I received the medicine 6 days after he sent it, i took the medicine as prescribed by him. Before I completed the medication the symptoms stopped. I went to the doctor and carried out another blood test, surprisingly I was Negative. I haven’t had any symptoms anymore. Dr. Dawn is great and you can
    contact on WhatsApp: +2349046229159
    Gmail ( dawnacuna314@gmail.com )

    If you need herbal medicine to cure any chronic or sexual transmitted disease's like.
    HERPES.
    CANCER.
    HIV/AID'S and more

    ReplyDelete