ABOUT UDOMSSO

The University of Dodoma Sociology Students' Organization (UDOMSSO) is an academic and social organization which is under the department of Sociology and Anthropology in the College of Humanities and Social Sciences.

MISSION

Our mission is to Organize, Coordinate and Facilitate all activities relating to our areas of interest for social progress.

VISSION

UDOMSSO has a vission to become an effective students' organization and to spearhead for a positive community for both academic and social matters which affect students' daily life and the community at large.

Translate

Tuesday, 16 May 2017

YANGA YATWAA UBINGWA KWA MARA YA TATU MFULULIZO


Klabu ya soka ya Yanga ya Dar es salaam leo imetwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuifunga klabu ya Toto African ya Mwanza kwa goli moja bila majibu. Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Taifa, zilishuhudiwa timu zote zikicheza soka zuri huku kila mmoja akitambua umuhimu wa mechi hiyo. Wakati Yanga wakitaka kujihakikishia ubingwa, Toto African wao walikuwa wakipambana kufa na kupona ili kuhakikisha wanasalia katika
ligi na kushiriki ndani ya msimu unaokuja. 

Dakika 45 za awali ziliisha huku milango ikiwa migumu kufunguka kwa kila mmoja na hata zilipoongezwa dakika kadhaa bado matokeo yalikuwa ni 0-0. 

Kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi huku presha ya mchezo ikizidi kuongezeka kadri dakika zilivyozidi kwenda huku yanga waliwa wameutawala mchezo kwa asilimia nyingi zaidi ya Toto African. Ilibidi Yanga wasubiri hadi dakika ya 80 Tambwe alipopiga kichwa murua cha mpira uliopigwa krosi na beki wa pembeni wa Yanga Juma Abdul Jaffari na kuukwamisha mpira huo gorini akimwacha golikipa na mabeki wa Toto Africa wasijue cha kufanya. Hadi mwisho wa mchezo goli lilikuwa moja kwa Yanga huku Toto African wakitoka patupu. 

Pamoja na kwamba ligi haijaisha lakini wapinzani wa Yanga kwenye mbio za ubingwa "Simba", wanahitaji miujiza mikubwa kuibuka mabingwa kwani hata kama Yanga watafungwa mechi yao moja iliyobaki na Simba wakaibuka na ushindi, watakuwa na pointi sawa. Kitakachoibeba Yanga ni uwiano wa magoli ya kufunga na kufungwa huku Yanga ikiwa na wastani mzuri. Kwa maana hiyo Simba itaiombea Yanga ifungwe mechi ya mwisho huku yenyewe (Simba) ikishinda magoli zaidi ya 13. Katika akili za kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani japo mpira wa miguu una maajabu yake. Ubingwa huu ni wa mara ya tatu mfululizo na ni ubingwa wa mara ya 27 katika ligi kuu Tanzania bara na kuwa klabu pekee ambayo imetwaa makombe mengi zaidi ya ligi hiyo. HONGERA KLABU YA YANGA KWA UBINGWA WA MARA YA TATU MFULULIZO NA WA MARA YA 27 KATIKA LIGI KUU BARA.

No comments:

Post a Comment